Posts

Showing posts from June, 2018

NAFASI ZA KUJIUNGA NA CHUO CHA UDAKTARI .

Image
Chuo cha msongola health training institute. Kinatangaza nafasi za kujiunga na masomo Kwa mwaka 2018-2019.  kwa kozi za afya ngazi ya cheti na astashahada .  Chuo kipo mkoa dar -es -salaam wilaya ya ilala chuo kimesajiliwa na NACTE.  CHUO kina mazingira mazuri ya kujisomea na kina hostel kwa wasichana na wavulana       Chuo kina vifaa vya kisasa kwa jiri yakufundiahia.    Timiza malengo yako yakuwa daktari .na Msongola health training institute.                                      KOZI ZITOLEWAZO. Technician Certificate in Clinical Medicine- NTA Level 5 Ordinary Diploma in Clinical Medicine- NTA Level 6 Basic Technician Certificate in Community Health Contact us  Msongola Health Training Institute (MHTI) P.O Box 38112 Dar Es Salaam,Tanzania http://www.msongolainstitute.ac.tz/   Call us: Principal/CEO Dr. Alex...

STORY TAMU YA MAPENZI. **JAMANI BABA -3 mh...!!!!!

Image
story : Jamani baba-3 Mtunzi: Raphaely mwaluko Waliongea sana mwisho Christian alikubali kuwa na mahusiano ya kimapenzi na walipatana jinsi ya kuendesha mapenzi yao bila mtu yoyote kujua (ingawa waswahili wanasema hakuna siri ya watu wawili) Mzee Edwin siku hiyo alimnunulia zawadi nzuri sana mwanae Christina, Christina alifurahi sana kupewa zawadi na baba yake ilikuwa ni simu nzuri aina ya  LG  ya kisasa, haraka Christina aliingia ndani na kujiunga na huduma ya whasApp na kuanza kuchati na mpenzi wake Christian ambaye yeye tayari alikuwa na simu yenye whasApp, lakini gafla alikumbuka na kitu na kutoka chumbani kwenda sebuleni, aliikuta simu ya baba yake pale na kuichukua alifungua kwenye meseji hakuamini alichokutana nacho, akabaki akiduwaa asiamini……….. meseji iliandikwa hivi………… Baby nimemiss penzi lako tamu ulilonipa jana kama itawezekana na leo nataka tena, kwani wewe hujanimiss mpenzi wangu jamani!!! Ilikuwa ni meseji toka kwa rafiki mkubwa wa mama yake, Kha...

mh.Tundu lissu kesho afanyiwa upasuaji mwingine aongea haya kwa watanzania.

Image
MBUNGE  wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu kesho Juni 4, 2018 atafanyiwa upasuaji wa 21 wa kuunga goti la mguu wake wa kulia huku akiwataka Watanzania kumuombea. Upasuaji huo ni mwendelezo wa upasuaji ambao amekuwa akifanyiwa katika Hospitali ya Nairobi nchini Kenya alikokuwa amelazwa baada ya kushambuliwa kwa risasi akiwa katika makazi yake mjini Dodoma Septemba 7, 2017. Alipatiwa huduma za awali katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma. Lissu ameeleza hayo leo Jumapili Juni 3, 2018 kupitia taarifa aliyoitoa katika ukurasa wa mtandao wa kijamii wa Instagram, akiambatanisha na picha yake akiwa amelala wodini kando ya mkewe, Alicia. “Hello  wapendwa wangu. Ninaamini wengi wenu, kama sio wote, mnafahamu kwamba Jumatatu Juni 4 nitafanyiwa operesheni ya mwisho kwenye mguu wa kulia,” amesema. “Ni operesheni kubwa inayotazamiwa kuchukua takriban saa nane kwa taarifa nilizopewa tangu mwanzoni mwa wiki hii. Hivyo madaktari wangu wametumia muda...

RAIS MAGUFULI ASIKITISHWA NA KIFO CHA MAPACHA WAWILI WALIO KUWA WAMESHIKANA.

Image
Leo June 3, 2018 Rais Dkt. John Pombe Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa familia, Masista wa Maria Consolata na wote walioguswa na kifo cha mabinti mapacha walioungana Maria na Consolata Mwakikuti waliofariki dunia jana jioni katika hospitali ya Mkoa wa Iringa. Rais Magufuliwa aliwatembelea Maria na Consolata walipokuwa wakipata matibabu katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Jijini Dar es salaam January 6, 2018. Pamoja na kuwapa pole Maria na Consolata waliongoza sala ya kuliombea Taifa na Viongozi wake. Rais Magufuli anasema anatambua kuwa Maria na Consolata walikuwa na ndoto kubwa ya kuja kulitumikia Taifa baada ya kumaliza Chuo Kikuu cha Masista wa Consolata Ruaha (RUCO) walikokuwa wakiendelea na masomo yao, lakini haikuwa hivyo.

BREAKING NEWS :- Bodi ya mikopo yasitisha utoaji mikopo kwa stashahada.

KUSITISHA MIKOPO KWA WANAFUNZI WA STASHAHADA (DIPLOMA) Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) inapenda kuutaarifu umma kuwa imesitisha mpango wa kutoa mikopo kwa wanafunzi wanaosoma  stashahada (Diploma) kuanzia mwaka wa masomo 2018/2019  kama ilivyotangaza awali. Itakumbukwa kuwa tarehe  10 Mei  mwaka huu, HESLB ilitoa mwongozo unaosimamia utoaji mikopo kwa mwaka wa masomo 2018/2019 . Mwongozo huo, pamoja na mambo mengine, unaeleza kuwa HESLB itaanza kutoa mikopo kwa wanafunzi wa stashahada na kuwa mwongozo kuhusu utaratibu wa kuomba mikopo hiyo ya wanafunzi wa stashahada ungetolewa baadae. Hatua hii imechukuliwa ili kuhakikisha kuwa kiasi chote cha  TZS 427.5 bilioni zilizotengwa kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi kwa mwaka  2018/2019 zinaelekezwa kwa wanafunzi wenye mikopo hivi sasa na waombaji wapya wahitaji ambao wana sifa za kujiunga na kozi za shahada tu ambao ndiyo walengwa wakuu. Hivyo basi, tunatoa wito kwa wanafuzi wote wenye ...

NJIA ZA KUJIKWAMUA UTOKE KATIKA UMASIKINI.

Image
Kila wakati ninapopata nafasi ya kuzungumza na watu juu ya maisha nimekuwa nikilisema hili mara kwa mara kuwa maisha tunayoishi yanaongozwa na kanuni. Kanuni hizi ndizo zinazoleta matokeo ya aina fulani katika maisha yetu kila siku uwe unajua au hujui. Kiuhalisia kutokana na kanuni hizi au njia hizi wale wanaofanikiwa hujikuta ndio wanaomudu kutumia kanuni hizi vizuri katika maisha yao na wale wasiofanikiwa na kuishia kwenye umaskini hujikuta wao ndio wanaoshindwa kutumia kanuni au njia hizi ndogo ndogo katika maisha yao. Ni kweli kama unataka kufanikiwa na kutoka kwenye umaskini ulionao ni lazima  utumie njia hizi ambazo zitakusaidia sana katika mchakato mzima wa kupata utajiri katika maisha yako. Hizi ni njia ambazo zimetumiwa na watu mbalimbali waliofanikiwa kuwatoa kwenye umaskini na hatimaye kuwa matajiri. Kwa kadri utakavyomudu kutumia njia hizi za mafanikio utakuwa unajitengenezea uwezo mkubwa wa kufanikiwa kwa kile unachofanya. Njia hizi ni zipi ambazo zinawe...

HIMIDI AIAGA AZAM FC KWA UCHUNGU NA KUTIMKIA MISRI

Image
Aliyekuwa nahodha wa klabu ya soka ya Azam FC, Himid Mao ameiaga klabu hiyo rasmi baada ya kusaini kuichezea timu ya Petrojet ya Misri huku akiiomba msamaha timu hiyo na zaidi kueleza namna timu hiyo ilivyompokea akiwa kijana mdogo hadi leo amekuwa mtu mzima. ''Nimeishi kama mwana familia kwa miaka yote nilikuja nikiwa kijana mdogo kabisa wa kidato cha kwanza naondoka nikiwa nimepevuka kimwili na kiakili, mimi ni binadamu kama kuna sehemu niliwakosea naombeni mnisamehe na mimi nimesamehe kama mlinikosea'', ameandika. Aidha Himid pia amewashukuru viongozi wa timu hiyo kwa kuwa imara katika nyakati zote walipokuwa wanafanya vizuri na hata walipofanya vibaya waliwapa moyo na kuwajenga ili wafanye vizuri. Licha ya viongozi wa wana lambalamba kutaka kumbakiza lakini Himid ameeleza aliwaomba akatafute changamoto mpya hivyo ilibidi wamkubalie ombi lake na tayari viongozi wamethibitisha kumaliza naye kwa amani huku wakimtakia kila la kheri. Himid Mao amesaini mkataba ...

SIMULIZI TAMU YA MAPENZI.

Image
Wakati mwanamfalme wa Kiafrika na karani mmoja mwanamwali Mzungu wa maisha ya wastani kutoka kwa wamiliki wa bima wa Lloyd, walipoamua kuoana mnamo mwaka 1948, ilichochea hisia mbalimbali nchini Uingereza na Afrika. Seretse Khama alikutana na Ruth Williams alipokuwa mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha Oxford na wakaanza kuchumbiana. Baada ya masomo yake, alitarajiwa kwenda nyumbani hadi katika taifa lake lililokuwa koloni ya Uingereza wakati huo ikijulikana kama Bechuanaland ambayo sasa ni Botswana, na kuoa mmoja wa watu wa kabila lake, lakini mapenzi yake kwa Williams ya libadilisha kila kitu. Familia yake ilipinga ndoa hiyo na Khama akalazimika kukatalia mbali fursa ya kuwa mfalme. Serikali ya Uingereza iliingilia kati na kujaribu kupinga ndoa hiyo haua iliyomfanya Khama kufukuzwa kutoka nchi yake. Askofu wa London, William Wand, angeruhusu tu harusi inayofanyika kanisani ikiwa tu utawala nchini Uingereza ungeruhusu ndoa hiyo kufanyika. Hilo halikufanyika. Wapenzi hao waw...

KUNAFAIDA KUBWA YAKUMTUMIKIA MUNGU WAKATI WA UJANA.

Image
FAIDA YA KUMTUMIKIA MUNGU KATIKA UJANA (Pastor Shenyagwa, KAMBI YA VIJANA 16 Jan 16) Yeremia 1:4-6   Yeremia aliitwa kumtumikia Mungu tangu akiwa  mdogo Mungu mahali pengi aliita watumishi wengi tangu wakiwa vijana. I Samweli 16:13      I Samweli 3:1          Isaya 6:5       Waamuzi 6:1 Vijana wengi hukataa wanapoitwa hujiona wadhaifu.Changamoto walizo nazo wanapoitwa ni kujiona wadogo, dhaifu, wanyonge, hawataweza, ni duni n.k Kwa nini Mungu aite watu tokea ujanani? Hutaka kumtengeneza huyu kijana kabla hajaanza kumtumia Yeremia 1:9 Hutaka kumtakasa kabla ya kumtumia Isaya 6:5-6 Hutaka akufundishe vya kutosha Kutoka 3 Mungu kabla ya kukutumia atakufundisha na ataendelea kukufundisha Chunguza safari yako Tambua uwepo wa “Eli” wako. Baba wa kiroho hukuwezesha kuijua sauti ya Mungu ili uweze kumtumikia. Hakuna mafanikio katika utumishi wako ka...

STORY YA MAPENZI

Image
SIMULIZI ZA MAPENZI SIMULIZI FUPI ,,,LOVE STORY Kijana mmoja alitokea kumpenda sana dada mmoja ijapokuwa dada huyo alikuwa akimtolea nje mara kwa mara lakini kijana hakukata tamaa, akiendelea kurusha ndoano huku akiamini siku moja atafanikiwa.Siku moja dada huyo akiwa yupo nyumbani aliamua kumpigia simu huyu kaka na kumtaka aje nyumbani kwake, yule kijana alifurahi na kuhisi sasa ombi lake limekubaliwa. Akiwa nyumbani kwake dada huyo , alikuwa amevalia kanga moja laini, kutokana na hali ya hewa ya joto la Dar es salaam.Kwa upande wa yule kijana alikuwa amefurahi sana na haraka alijiandaa na kuanza safari kuelekea kwa huyu dada, njia ni kaka huyu alikuwa akijiuliza maswali mengi, huku akiwa haamini kama yule dada amemuita nyumbani kwake. Alipofika, alibisha hodi na yuel dada akafungua mlango huku akionyesha tabasamu pana katika paji la uso wake. Kaka huyu aliingia ndani huku kijasho kikimteremka mithili ya mtu aliyekuwa anakimbia. Dada huyu alimkaribisha vizuri, yule kaka aliomba maji...