Posts

     MSONGOLA HEALTH TRAINING INSTITUTE.   Chuo kimesajiliwa na NACTE  REG/HAS/178P Chuo kinatangaza nafasi za masoma kwa mwaka wa masomo 2018/2019                    Kozi zitolewazo ni:- 1.Basic techinician  certificate in clinical medicine   NTA Level 4 2.Technician certificate in clinical medicine NTA Level 5 3.Ordinary diploma in clinical medicine NTA level 6   SIFA ZA MUOMBAJI. -Awe amemaliza kidato cha NNE na awe na ufauru katika masomo ya sayansi angalau  physics -D chemistry -D Biology -D basic mathematics -D  (CERTIFICATE ) - Kwa wale walio hitimu kidato cha sita  Wataanza na DIPLOMA NTA level 6 Chuo kina HOSTEL kwa wavulana na wasichana kwa wale wote wanao toka mikoa ya mbali .   CHUO KIPO MKOA WA DAR-ES - SALAAM WILAYA YA ILALA  KINA MAZINGIRA MAZURI NA VIFAA VYA KISASA KWA KUFUNDISHIA PIA USAFIRI KWA WANAFUNZI WOTE.     ...

NAFASI ZA KUJIUNGA NA CHUO CHA UDAKTARI .

Image
Chuo cha msongola health training institute. Kinatangaza nafasi za kujiunga na masomo Kwa mwaka 2018-2019.  kwa kozi za afya ngazi ya cheti na astashahada .  Chuo kipo mkoa dar -es -salaam wilaya ya ilala chuo kimesajiliwa na NACTE.  CHUO kina mazingira mazuri ya kujisomea na kina hostel kwa wasichana na wavulana       Chuo kina vifaa vya kisasa kwa jiri yakufundiahia.    Timiza malengo yako yakuwa daktari .na Msongola health training institute.                                      KOZI ZITOLEWAZO. Technician Certificate in Clinical Medicine- NTA Level 5 Ordinary Diploma in Clinical Medicine- NTA Level 6 Basic Technician Certificate in Community Health Contact us  Msongola Health Training Institute (MHTI) P.O Box 38112 Dar Es Salaam,Tanzania http://www.msongolainstitute.ac.tz/   Call us: Principal/CEO Dr. Alex...

STORY TAMU YA MAPENZI. **JAMANI BABA -3 mh...!!!!!

Image
story : Jamani baba-3 Mtunzi: Raphaely mwaluko Waliongea sana mwisho Christian alikubali kuwa na mahusiano ya kimapenzi na walipatana jinsi ya kuendesha mapenzi yao bila mtu yoyote kujua (ingawa waswahili wanasema hakuna siri ya watu wawili) Mzee Edwin siku hiyo alimnunulia zawadi nzuri sana mwanae Christina, Christina alifurahi sana kupewa zawadi na baba yake ilikuwa ni simu nzuri aina ya  LG  ya kisasa, haraka Christina aliingia ndani na kujiunga na huduma ya whasApp na kuanza kuchati na mpenzi wake Christian ambaye yeye tayari alikuwa na simu yenye whasApp, lakini gafla alikumbuka na kitu na kutoka chumbani kwenda sebuleni, aliikuta simu ya baba yake pale na kuichukua alifungua kwenye meseji hakuamini alichokutana nacho, akabaki akiduwaa asiamini……….. meseji iliandikwa hivi………… Baby nimemiss penzi lako tamu ulilonipa jana kama itawezekana na leo nataka tena, kwani wewe hujanimiss mpenzi wangu jamani!!! Ilikuwa ni meseji toka kwa rafiki mkubwa wa mama yake, Kha...

mh.Tundu lissu kesho afanyiwa upasuaji mwingine aongea haya kwa watanzania.

Image
MBUNGE  wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu kesho Juni 4, 2018 atafanyiwa upasuaji wa 21 wa kuunga goti la mguu wake wa kulia huku akiwataka Watanzania kumuombea. Upasuaji huo ni mwendelezo wa upasuaji ambao amekuwa akifanyiwa katika Hospitali ya Nairobi nchini Kenya alikokuwa amelazwa baada ya kushambuliwa kwa risasi akiwa katika makazi yake mjini Dodoma Septemba 7, 2017. Alipatiwa huduma za awali katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma. Lissu ameeleza hayo leo Jumapili Juni 3, 2018 kupitia taarifa aliyoitoa katika ukurasa wa mtandao wa kijamii wa Instagram, akiambatanisha na picha yake akiwa amelala wodini kando ya mkewe, Alicia. “Hello  wapendwa wangu. Ninaamini wengi wenu, kama sio wote, mnafahamu kwamba Jumatatu Juni 4 nitafanyiwa operesheni ya mwisho kwenye mguu wa kulia,” amesema. “Ni operesheni kubwa inayotazamiwa kuchukua takriban saa nane kwa taarifa nilizopewa tangu mwanzoni mwa wiki hii. Hivyo madaktari wangu wametumia muda...

RAIS MAGUFULI ASIKITISHWA NA KIFO CHA MAPACHA WAWILI WALIO KUWA WAMESHIKANA.

Image
Leo June 3, 2018 Rais Dkt. John Pombe Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa familia, Masista wa Maria Consolata na wote walioguswa na kifo cha mabinti mapacha walioungana Maria na Consolata Mwakikuti waliofariki dunia jana jioni katika hospitali ya Mkoa wa Iringa. Rais Magufuliwa aliwatembelea Maria na Consolata walipokuwa wakipata matibabu katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Jijini Dar es salaam January 6, 2018. Pamoja na kuwapa pole Maria na Consolata waliongoza sala ya kuliombea Taifa na Viongozi wake. Rais Magufuli anasema anatambua kuwa Maria na Consolata walikuwa na ndoto kubwa ya kuja kulitumikia Taifa baada ya kumaliza Chuo Kikuu cha Masista wa Consolata Ruaha (RUCO) walikokuwa wakiendelea na masomo yao, lakini haikuwa hivyo.

BREAKING NEWS :- Bodi ya mikopo yasitisha utoaji mikopo kwa stashahada.

KUSITISHA MIKOPO KWA WANAFUNZI WA STASHAHADA (DIPLOMA) Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) inapenda kuutaarifu umma kuwa imesitisha mpango wa kutoa mikopo kwa wanafunzi wanaosoma  stashahada (Diploma) kuanzia mwaka wa masomo 2018/2019  kama ilivyotangaza awali. Itakumbukwa kuwa tarehe  10 Mei  mwaka huu, HESLB ilitoa mwongozo unaosimamia utoaji mikopo kwa mwaka wa masomo 2018/2019 . Mwongozo huo, pamoja na mambo mengine, unaeleza kuwa HESLB itaanza kutoa mikopo kwa wanafunzi wa stashahada na kuwa mwongozo kuhusu utaratibu wa kuomba mikopo hiyo ya wanafunzi wa stashahada ungetolewa baadae. Hatua hii imechukuliwa ili kuhakikisha kuwa kiasi chote cha  TZS 427.5 bilioni zilizotengwa kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi kwa mwaka  2018/2019 zinaelekezwa kwa wanafunzi wenye mikopo hivi sasa na waombaji wapya wahitaji ambao wana sifa za kujiunga na kozi za shahada tu ambao ndiyo walengwa wakuu. Hivyo basi, tunatoa wito kwa wanafuzi wote wenye ...

NJIA ZA KUJIKWAMUA UTOKE KATIKA UMASIKINI.

Image
Kila wakati ninapopata nafasi ya kuzungumza na watu juu ya maisha nimekuwa nikilisema hili mara kwa mara kuwa maisha tunayoishi yanaongozwa na kanuni. Kanuni hizi ndizo zinazoleta matokeo ya aina fulani katika maisha yetu kila siku uwe unajua au hujui. Kiuhalisia kutokana na kanuni hizi au njia hizi wale wanaofanikiwa hujikuta ndio wanaomudu kutumia kanuni hizi vizuri katika maisha yao na wale wasiofanikiwa na kuishia kwenye umaskini hujikuta wao ndio wanaoshindwa kutumia kanuni au njia hizi ndogo ndogo katika maisha yao. Ni kweli kama unataka kufanikiwa na kutoka kwenye umaskini ulionao ni lazima  utumie njia hizi ambazo zitakusaidia sana katika mchakato mzima wa kupata utajiri katika maisha yako. Hizi ni njia ambazo zimetumiwa na watu mbalimbali waliofanikiwa kuwatoa kwenye umaskini na hatimaye kuwa matajiri. Kwa kadri utakavyomudu kutumia njia hizi za mafanikio utakuwa unajitengenezea uwezo mkubwa wa kufanikiwa kwa kile unachofanya. Njia hizi ni zipi ambazo zinawe...